eRRy, ♀♂Inc.

The Love Blog

Akiwa na sifa hizi ruksa kumuoa


Naomba kuchukua nafasi hii kuwakumbusha wasomaji wangu wapenzi kwamba kitabu changu cha True Love (Penzi la Dhati) kinapatikana mitaani kwa wauza magazeti wote. Ni kitabu chenye mada nzuri za mapenzi, pamoja na love sms (ujumbe wa mahaba) kali kwa ajili ya kumtumia yule unayempenda! Baada ya hayo, sasa tunageukia mada yetu ya leo, nazungumzia kuhusu sifa za mwanamke anayefaa kuwa mke bora.

Katika mambo muhimu ambayo unapaswa kuelekeza akili yako yote katika kufanya maamuzi ni pamoja na mapenzi! Ukioa mwanamke ambaye unadhani unampenda au ukaolewa na mwanaume ambaye unadhani unampenda kumbe sio hivyo, au baada ya kuingia katika ndoa ukakutana na mambo mengine ambayo hukuyategemea, uwezekano wa kuharibu maisha yako na kuona mapenzi machungu huwa mkubwa sana!

Katika kufanya uchaguzi wa mwenzi wa maisha ni lazima uwe makini sana. Sasa linapokuja suala la kuwa na mke mwema, ni lazima ujue sifa anazotakiwa kuwa nazo. Kama unataka kuoa lazima mwanamke huyo awe na sifa zifuatazo:

HANA TAMAA...
Mwanamke anayefaa kuolewa ni lazima asiwe na tamaa, awe anaridhika na kile kidogo anachopewa na mpenzi wake. Kutamani kila kitu au kutaka vitu vikubwa ni tatizo kubwa sana katika ndoa. Ikiwa upo katika uhusiano na mwanamke mwenye tamaa, anza kujiuliza mara mbili.

Mchunguze vizuri utakuja kugundua nia yake ni kukuchuna tu na sio kuishi na wewe katika ndoa. Huo ndiyo ukweli ambao upo hata kama utakuumiza.

HAEHESABU MAKOSA
Hii ni kati ya sifa za mwanandoa bora, ili uwe mwanandoa kamili lazima uwe na ‘kifua’, sio kila kitu unanung’unika na kuanika nje! Kuanzia mnapokuwa marafiki, anza kumchunguza mchumba wako, ukimkosea na kumuomba msamaha, akishakusamehe hurudia tena kukuuliza? Ukiona anafanya hivyo, tambua kuwa huyo sio mke bora.

Mwanamke mwema siku zote huangalia mbele, sio ukifanya kitu kidogo tu, anaanza kukuuliza juu ya makosa yako ya nyuma; “Kila siku unaomba msamaha, wewe ni mwanaume wa aina gani? Mara ya kwanza uliniomba msamaha nikakubali, ukarudia tena nikakubali leo tena, ah nimechoka!” Haya ni baadhi ya maneno ambayo hutumiwa na wanawake wa aina ninayoizungumzia katika mada hii. 

MOYO WAKO URIDHIE!
Hii isibaki kuwa hadithi za kufikirika, iwe yakini na moyo wako uzungumze hivyo, kuwa unampenda kwa mapenzi ya dhati! Utajuaje kama unampenda? Sema na moyo wako utakupa ukweli juu ya hilo, usikurupukie mapenzi, usije ukamuona msichana siku moja amevaa suruali inambana kiasi cha kuonyesha umbile lake halafu ukamtamani ukadhani unampenda, utakuwa unapotoka!

Mapenzi sio kitu cha mchezo, huanza moyoni jiridhishe kwanza ndipo ukubali kumwingiza katika moyo wako. Kumbuka kitu kimoja, unapoamua kufunga ndoa na mtu ni ahadi ambayo mmeahidiana mbinguni na duniani, ni ahadi ambayo inapaswa kutenganishwa na kifo tu, sio vinginevyo! Kamwe usifanye majaribio katika mapenzi, mapenzi hayajaribiwi!

NI KWELI ANAKUPENDA?
Hili ni muhimu kuliko la kwanza, ingawa ni vizuri kuishi na mwanamke unayempenda lakini pia ni lazima awe anakupenda! Sio vigumu sana kumfahamu mwanamke anayekupenda, lakini pia inawezekana ukaona anakupenda kumbe ni danganya toto!

Kimsingi katika hili ni lazima utumie akili yako yote uweze kutambua hilo. Mwanamke anayekupenda huwa mvumilivu, anayekusikiliza pia mwenye kuwajali ndugu, marafiki na jamaa zako! Hii ni alama nzuri ya kuwa na mke mwema anayekubalika na ndugu zako pamoja na rafiki zako wa karibu.

MWEREVU...
Siyo lazima awe na elimu ya darasani, haijalishi ni mwanamke aliyekulia kijijini au mjini, lakini hapa tunaangalia uwezo wake wa kufikiri, ni mwerevu? Anayejua mambo na njia za kuyatatua? Hili ni jambo la msingi sana kulifahamu.
Hata hivyo, inategemea wewe umepanga kuishi na mwanamke wa aina gani, lakini mwanamke ninayemzungumzia hapa ni yule mwenye uwezo wa kutosha wa kufikiri na kupambanua mambo!

Mwenye uwezo huu ni yule ambaye ukimwambia kuwa kibanda chako unachofanyia biashara Kariakoo kimevunjwa na Askari wa Jiji, atakuwa na ushauri wa kukupa utakaokusaidia kuendesha maisha yako na sio kukulaumu au kuishia kukusikitikia bila kuwa na wazo la kukupa. Kusikitika kwake hakumaanishi kuwa yupo pamoja na wewe, atakuwa pamoja na wewe pale atakapoonyesha njia nyingine ya kukusaidia kujikwamua kimaisha.

Sio kuishia mizinga kila siku, mara simu haina dola, mara mama Juma amepitisha vitenge anakopesha, lazima uangalie je, unapokwama anakuwa pamoja na wewe kifikra au ni mzigo wa mananasi? Hilo ni la kuzingatia sana katika maisha ya sasa.

Mwanamke wa aina hii unapaswa kumchunguza mapema ili usije ukaoa mzigo! Suala la uwezo wa kufikiri lina umuhimu mkubwa sana katika maisha ya sasa, ni bora mkakosa mali lakini mkawa na uwezo wa kufikiri na kutatua matatizo mbalimbali ya kimaisha. Huu ndio ukweli ingawa wengi wanaukwepa! Nawasilisha.

Lazima uwe makini wakati wa kutafuta mke!

Tunaangalia umakini wakati wa kumtafuta mke mwema, ni wiki ya nne sasa tunaangalia sifa za mwanamke anayefaa kuwa mke. Kimsingi sio kila mwanamke anafaa kuwa mke! Unaweza kuwa mwanamke, lakini usiwe mke! Hii ndio sababu nachambua mada mbalimbali za kuweza kupata wenzi sahihi wa maisha. 

Katika mada hii, bila shaka wanaume wanapata nafasi ya kuweza kuwatambua wenzi sahihi wa maisha, lakini pia wanawake wanapata nafasi ya kutoka katika sehemu waliyopo ambayo napenda kuiita gizani na kurudi kwenye nuru ili waweze kupata wenzi wa maisha yao.

Hebu sasa tuendelee na vipengele vinavyofuata…

ANAYEJALI USAFI!
Kama ni mchafu atakuwa mwanamke wa aina gani? Maana tumezoea kusikia kila wakati kuwa mwanamke ni pambo la nyumba, sasa atawezaje kuwa pambo la nyumba wakati ni mchafu? Hili sio suala la kufundishana, ni hulka ya mtu ambayo huzaliwa nayo.

Jaribu kuvuta picha, umetoka kazini ukiwa umeongozana na rafiki zako. Kwa mbwembwe zote unataka kuwakaribisha nyumbani kwako. 

Unafika unamkuta mtoto kajisaidia haja kubwa mlangoni, tena anachezea kinyesi chake mwenyewe, mkeo hana habari kabisa, amekaa kwenye jamvi yupo bize anapiga soga na shoga zake, akiwa mchafu! Atakuwa mke kweli huyo au matatizo?

Sifa ya mwanamke ambayo karibu wote hupaswa kuwa nayo, ni pamoja na usafi. Usafi ni kitambulisho cha mwanamke. 
Kama asipokuwa msafi, ni rahisi familia yako kushambuliwa na magonjwa ya mlipuko. Ni lazima mkeo awe msafi.

ANAKUHESHIMU...
Hili sio ombi, ni amri! Mwanamke anapaswa kumheshimu mumewe, sasa dalili za heshima huanza kuonekana tangu mapema wakati wa uchumba. 

Kama upo katika uhusiano na mwanamke ambaye hana heshima, ni dalili za kupata mke asiye na heshima. Tabia hii nayo haibadilishiki, ni lazima uwe makini sana na mwanamke wa aina hii.

Dalili ya kwanza ambayo unaweza ukaiona ni kutojali unayomwambia, mathalani unamzuia kuvaa nguo ya aina fulani halafu analazimisha kuvaa, hilo ni tatizo na usitegemee atabadilika mkiwa ndani ya ndoa. Atakuwa tatizo zaidi na zaidi! Sasa usikubali kufuga matatizo. 

ANAJALI NASABA YAKO!
Ili awe mke kamili atakayefaa ndani ya nyumba lazima awe na sifa hii! Asiishie kusema kuwa anakupenda wewe lakini ndugu zako anawadharau, hayo sio mapenzi. Lazima aonyeshe kukujali wewe na ndugu pamoja na jamaa zako, hayo ndio mapenzi ya dhati yanayopaswa kuwa nayo mwanamke mwema.

Hilo linaweza kuonekana kuanzia siku utakayomtambulisha kwa rafiki zako wa karibu. Kama ni kweli anakupenda na ana nia ya kuishi na wewe katika maisha yake yote, atakubali kuwa na ndugu zako, kushirikiana nao kwa kila kitu, na kuwajali kama wewe!

Ukimwambia akae na mama yako kwa kuwa ni mgonjwa hapaswi kukataa, akifanya hivyo ujue kuna tatizo hapo! Kama hatampenda mama yako ambaye amekuleta duniani, atampenda nani zaidi? Pambanua mwenyewe!

USIKUBALI KUSHINIKIZWA!
Pamoja na yote niliyoandika lakini hivi sasa kuna tabia moja ambayo sio nzuri, iliyopo kwa baadhi ya jamii yetu, kushinikiza! Kamwe usikubali kuishi na mwanamke ambaye unaamini huna mapenzi naye. 

Kama wazazi wako wanalazimisha jambo hilo, ni vizuri ukakaa na kuzungumza nao kwa undani na uwaeleze athari za kuishi na mwanamke ambaye hujampenda.

Hili ni rahisi kidogo, kwa kuwa unaweza ukazungumza na wazee ambao wataweza kufikisha ujumbe huu kwa wazazi wako. Kuishi na mwanamke usiyempenda ni matatizo, unaweza ukajikuta ukimfanyia vituko mtoto wa watu bure! Zungumza na wazazi wako!

ANGALIZO KWA WANAWAKE
Wewe msichana unayesoma mada hii unapaswa kubadilika! Wanaume waoaji siku hizi ni wachache sana. Kumbuka kuwa mwanamke anapoolewa ni heshima kwake na familia nzima kwa ujumla, lilia heshima hiyo, usikubali kuishi bila heshima hii. Lakini ili uweze kuipata lazima uwe na sifa nilizozianisha kwa majuma manne mfululizo.

Kama ni kweli unataka kuingia kwenye ndoa, anza kufanya mabadiliko katika mienendo yako kuanzia leo. Jenga heshima katika maisha yako yajayo, anza kutengeneza njia za kuonwa mwanamke bora!

Kukosa mwenzi wa maisha, sababu na dawa

Nakufagilia msomaji wangu kwa kuichagua saafu hii kuwa dawa yako tosha katika uhusiano, kwa kutambua hilo, naahidi sitakuangusha.

Katika Championi Jumatatu, niliishia katika changamoto ya umalaya kama pointi nyingine ambayo huwakosesha watu wengi wenzi wa maisha, nilifafanua jinsi ambavyo wale wenye sifa hiyo hukabiliana na ugumu wa kupata wapenzi wa kweli.

Nafurahi ulinisoma, sasa tusonge mbele kwa mbele, Mungu yupo.

KUTOKUWA WAAMINIFU 
Hii ni changamoto nyingine ambayo huwasababishia watu wengi kukosa wenzi wao wa maisha, kila mtu anapenda kuwa na mpenzi anayeaminika ambaye hatompa jakamoyo la kila mara.

Staili ya maisha ya baadhi ya watu, yamewafanya kushindwa kuaminika, wanaishia kudharauliwa na kuonekana kama daraja fulani ambalo linaweza kulinganishwa na wahuni,

Hivyo basi, kama unataka ikuchukue wepesi kupata mwenzi wa maisha huna budi kujiangalia mwenendo wako, ujitathimini hatua kwa hatua tena kwa kwa umakini wa hali ya juu. Je umepata jawabu gani? Watu wanakuonaje? Hawakuhamini?

Jibu, ndiyo? Basi jirekebishe mara moja jiheshimu na uishi katika misingi inayokubalika ili jamii ikuamini. Kama wewe ni kiruka njia, maisha yako hayaeleweki, utaendelea kutazamwa kama katuni isiyo na tafsiri.

Hujulikani unafanya kazi wapi wewe ni mjanja mjanja tu, kila siku unaonekana na mpenzi mpya, watu wanakuhisi ni jambazi, muonekano wako ni wa kihuni, hali hiyo inakujengea mazingira magumu ya kupata mwenzi. Badilika ndugu!

UONGO
Wengi wamekuwa wakitumia ‘gia’ tofauti kupata wapenzi, hii huwatokea zaidi wanaume ingawa kuna baadhi ya akina dada nao huwa hawajambo kwa kusema uongo ili kujisafisha mbele ya viburudisho vyao.

Lakini ukweli umethibiti, njia ya muongo ni fupi au ndege mjanja huanaswa na tundu bovu pia wahenga walisema mbio za sakafuni huishia ukingoni.

Hivyo basi, utadanganya wawili watatu wa mwanzo, kwa ajili ya kukidhi matakwa yako, baadaye itakuwa wazi kwa kila mtu na atajua unavyotumia, akishakubaini mmoja basi na jamii yote itakujua, kwa kuwa habari husambaa mitaani.

Watu wakishaambiana, jua na thamani yako itashuka tu, kuporomoka kwa thamani ni wazi huheshimiwi na hiyo ni ishara kwamba unadharauliwa. 

Kwa mantiki hiyo itakuwaia vigumu kupata mwenzi wa kweli ambaye waweza kumfanya kuwa mke au mume.

MAPENZI YA MBALI
Fimbo ya mbali haiui nyoka, ndivyo wahenga walivyosema, lakini ngano hiyo ina ukweli wa asilimia nyingi mno, hujawahi kusikia watu wakinena ya kwamba ni wako akiwa kwako akitoka ne si wako?

Jibu, ndiyo basi huo ndiyo ukweli wa mapenzi ya watu wengi wa kisasa, ukiwa karibu na mwenzi wako ni rahisi kudumu naye kuliko kuwa naye mbali, si unajua tena “abiria chungu mzigo wako?”

Hata hivyo, ni ukweli kuwa wengi hujikuta wakiwa mbali na wapenzi wao kwa sababu za kikazi, kimasomo na nyinginezo hali hiyo huharibu mapenzi ya watu wengi.

Kuishi mbali na mwenzi wako huondoa uaminifu kwa sababu huzua chembechembe za usaliti, kwahiyo kama unataka mwenzi wako awe wa kudumu, unashauriwa kuwa naye karibu.

Natumaini ulikuwa sambamba na mimi tangu Jumatatu, wakati nilipoanza kuchambua mada hii, kwa maana hiyo nina uhakika kwamba umepata somo murua ambalo kwa 100% litakuwa limekupa mwongozo.

Unadhani bado nahitaji kukupa changamoto zaidi? Hapana ndugu, hizo zatosha!

Mambo ya kuzingatia kabla ya kuoa au kuolewa

            JE, UPO TAYARI KUWA MWANANDOA? 
Utayari ninaozungumzia hapa ni ule wa kujiandaa kikamilifu kisaikolojia na kukubaliana na hali hiyo ya kuwa ndani ya ndoa. Mwingine anaweza akaingia katika ndoa kwa sababu fulani naye yupo katika ndoa, au akaamua kuingia katika ndoa kwa sababu ya shinikizo la wazazi, haitakiwi hivyo, ni lazima uhakikishe wewe mwenywe upo tayari kuingia katika ndoa.

Usiingie katika ndoa kwa sababu una kazi, au umepata mafanikio fulani kimaisha! Hili linawasumbua wengi sana, baadhi ya vijana huingia katika ndoa baada ya kupata mafanikio katika maisha, wengi wao jambo la kwanza kuanza kulifikiria huwa ni kuoa, hili ni kosa, kwa kuwa utakuwa umeamua kuoa kwa sababu una pesa au mafanikio kimaisha lakini hukuwa umejipanga kikamilifu kwa ajili ya kuoa hasa kama hukuwa na mchumba hapo awali.

“Mimi sasa hivi mambo yangu yangu safi, hakuna jambo lingine la kufanya zaidi ya kuoa! Kama ni pesa ninayo, nyumba ninayo sasa nioe ili nitulie," kauli kama hii ni ya kawaida sana kwa baadhi ya vijana wenye fikra hii potofu. Pamoja na vijana kuwa na fikra hiyo, hebu angalia na wazazi wanavyokuwa na yao vichwani mwao; "Mwanetu sasa anajiweza kimaisha ni bora sasa akaoa, akioa atatulia na kujiepusha na umalaya!" Wazazi nao husema hayo.

Kimsingi ni kwamba suala la ndoa sio jambo dogo ambalo unaweza ukaamua haraka haraka bila kuwa na maandalizi ya kutosha kiali kabla. Unaweza ukajikuta umeoa mwanamke ambaye sio chaguo lako baada ya kuwa na pesa, lakini ukiingia ndani ya ndoa unakuta kumbe hakuwa mwanamke sahihi wa maisha yako. 

Unaweza ukapanga mambo yako kikamilifu kwanza kabla ya kuamua kuoa, usioe kwa sababu una pesa oa kwa sababu upo tayari kuingia katika ndoa. Bila shaka tayari umeshaelewa, mambo ya kuzingatia kabla ya kuingia katika ndoa.
Usikurupukie ndoa kabla ya kufanya uchunguzi wa kutosha.

Dondoo 10 za kumdatisha mpenzi wako!

UZUNGUMZAJI WAKO
Unavyozungumza na mpenzi wako ni tofauti kabisa na unavyozungumza na watu wengine. Ni hatari sana kutumia lugha ya ukali ama isiyo ya kiungwana kwa mpenzi wako. 

Unatakiwa kufahamu kwamba, mpenzi wako ni mtu muhimu sana katika maisha yako hivyo unatakiwa kuwa makini pindi unapozungumza naye.

Kuonesha kwamba wapo wasiojua mapenzi ni nini, unamkuta mtu anamwita mpenzi wake majina kama vile mshamba, demu, shembe na mengine mengine kama hayo. Mpenzi wako kweli umuite demu? Na wale wengine kule mtaani utawaita nani?

Huo si ustaarabu na kamwe mapenzi yenu hayawezi kushamiri kwa mtindo huo. Kuna wengine matusi hayawaishi midomoni mwao. Kwa kufanya hivyo jua tu kwamba unamboa laazizi wako.

Aidha mapozi katika uzungumzaji wako ni miongoni mwa vitu vinavyoweza kumdatisha mpenzi wako. Ukiwa na mpenzi wako usiongee kama chiriku au kama unagombana na mtu. Ongea kwa mapozi na hilo litamfanya akutofautishe wewe na watu wengine.

Kuna ambao wanapozungumza na wapenzi wao hawapitishi sentensi bila kutaja neno Dear ama Sweet. Hakika inavutia na ni mbolea tosha katika penzi la watu hao.

Lakini pia kuna baadhi ya maneno ambayo ukiyafanya kuwa sehemu ya maisha yako yanaweza kumvutia mpenzi wako. Kwa mfano neno NAKUPENDA! 

Hakuna asiyefurahia kupendwa hata kama ni mtoto mdogo, anafurahi sana kusikia neno 'Nakupenda' kutoka kwa watu wake wa karibu. Lakini linapokuja suala la mahusiano ya kimapenzi, neno hilo linachukua nafasi kubwa sana.

Ili kulifanya neno hilo kuwa na uzito wengine hulitamka kwa lugha ya kigeni yaani 'I love you Dear au sweet', ni sawa tu kwani maana ni ile ile. Huo ni mfano wa maneno ambayo ni chachu katika mapenzi.

Pia unatakiwa kuwa mwepesi wa kushukuru. Wengine hata wapenzi wao wajitahidi kuwafanyia mambo mazuri vipi, lakini ni wagumu sana kutamka neno ASANTE. 

Hata wanapowakosea wapenzi wao ni wagumu sana kuomba samahani. Kwa taarifa yako kama wewe ni mmoja wa wenye tabia hiyo elewa kwamba unamboa sana mpenzi wako.

Pia mnapokuwa faragha na mpenzi mkistarehe,baada ya kukufanyia kile ambacho roho yako imefurahi, mwambie asante kwa kukupeleka kwenye sayari mpya ya mahaba.
TABIA ZAKO

Huu ndio msingi imara wa uhusiano wa kimapenzi. Wapo wanawake ambao ni wazuri na wenye kila sifa ya kuwa na wapenzi bora, lakini kutokanana tabia zao chafu wamekuwa wakiachwa kila wanapoingia katika uhusiano.

Nani atakupenda na kudiriki kuendelea kuwa katika uhusiano na wewe kama tabia zako si nzuri? Wengi wetu tunapenda kupata sifa ya kuwapata wapenzi ama wachumba wenye tabia nzuri ili tuweze kusifiwa na marafiki zetu pamoja na wazazi. 

Kwa maana hiyo basi, kuwa makini sana na tabia ambazo unajua haziwezi kumvutia mpenzi wako ama jamii inayowazunguka kama vile WIVU uliopitiliza kiasi cha kuwa kero, kutaka makuu pamoja na tamaa zisizo na msingi.

Nimeweka wivu juu kutokana na ukweli kwamba, kuna wanawake hata wakiwakuta wapenzi wamesimama ama kupigiwa simu na mtu wa jinsia tofauti bila kujua ukweli wa mambo wanaanzisha vurumai, huu ni ulimbukeni.


JINSI UNAVYOMRIDHISHA
Yote hayo hapo juu ni tisa, lakini kumi ni jinsi unavyoweza kumridhisha mpenzi wako hasa mnapokuwa faragha mkipeana raha za dunia. 

Hata kama una tabia nzuri na umbile la kumvutia kiasi gani, kama huna utaalam na ujuzi wa kutosha katika kumpa raha mpenzi wako hasa linapokuja suala la tendo la ndoa, lazima penzi ama ndoa yako itakuwa na walakini.

Nilishawahi kusema huko nyuma kwamba, tunapozungumzia mapenzi hatumaanishi ngono. Ngono ama tendo la ndoa ni sehemu tu ya mapenzi ambayo haichukui nafasi kubwa sana kama baadhi yetu tunavyochukulia. 

Lakini kitu ambacho kimekuwa kikiwavutia walio wengi waume kwa wanawake ni utundu na ubunifu wakati mnapokuwa faragha. Kinachotakiwa ni kupeana kile roho inataka ili suala la kusalitiana lisiwepo. 

Mambo gani ‘humpagawisha’ boyfriend au girlfriend wako?

Unaishi na mpenzi ambaye humpendi? Upo katika uhusiano na mpenzi ambaye moyo wako hauna chembe ya mapenzi? Unadhani kuna mtu anakusumbua, anahitaji kuwa na wewe, lakini moyo wako hausemi chochote juu yake? Jibu lake ni rahisi sana, achana naye!

Ni uamuzi mgumu kidogo kuamulika tena kutoka kwa mshauri kama mimi, lakini kitaalamu, hupaswi kuwa na mpenzi ambaye humpendi! Ukiendelea kuwa naye kwa sababu za kimasilahi, kuna siku moja utalia! Utalia kwa kumkosa mpenzi wako baada ya kujiua atakapogundua kuwa huna mapenzi naye, au wewe unaweza ukapigwa au kupata madhara yoyote baada ya kufumaniwa na mtu mwingine.

Kimsingi sio busara kuwa katika uhusiano na mtu ambaye unaamini moyo wako haupo upande wake! Ishi na mpenzi ambaye usipomuona kwa saa kadhaa moyo wako unatetemeka, hayo ndiyo mapenzi! Kamwe usilazimishe kuishi na mtu kwasababu ana pesa, maarufu au shinikizo la mtu, moyo ukuthibitishie kuwa unamhitaji kweli awe wako.

Huo ni utangulizi tu, sasa tugeukie katika mada ya msingi ya leo, tunaangalia mambo yanayoweza kumfurahisha ‘kumpagawisha’ mpenzi wako. Kama upo na mpenzi ambaye unampenda kwa mapenzi ya dhati, lazima kila siku utakuwa ukifikiria umfanyie nini ili afurahi!

Huo ndiyo ukweli wa mapenzi ya dhati, sasa leo nataka kuzungumza zaidi na wale walio katika uhusiano ambao hawajaingia katika ndoa (boyfriend/girlfriend). 

Yapo mambo mengi ambayo huweza kumpagawisha mpenzi wako asikuchoke na siku zote akatamani kuwa na wewe. Ila nimekuandalia mambo muhimu zaidi kumi. Hebu tuanze kuyaangalia mambo hayo yanayoweza kumfurahisha mpenzi wako.


1. KUMFANYA MWENYE FURAHA
Kati ya mambo ambayo huweza kumpagawisha mpenzi na kumfanya ajisikie vyema muda wote, ni wewe kumfanya afurahi! Jiulize, kama wewe ndiyo mpenzi wake wa dhati wa moyo wake, unadhani ni nani anayepaswa kumfurahisha kila wakati kama sio wewe? Jibu mwenyewe…

Jambo la msingi ni wewe kujisogeza karibu yake kila wakati, yaani uwe sehemu ya maisha yake. Hilo linawezekana, unaweza kumtumia sms au waraka pepe akiwa kazini ukimtakia mchana mwema, kazi njema au mlo mwema. Ni kitu kidogo sana lakini kinachoweza kufanya uhusiano wenu uwe wenye furaha wakati wote.

2. MASHAMSHAM...

Umenisoma rafiki? Ninaposema mashamsham, namaanisha aina fulani ya mapenzi yenye vituko na michezo ya kimahaba! Ukiwa naye matembezini, usione haya kumshika mkono na wakati mwingine kumtania. Unaweza kumshika mkono na kuupapasa-papasa taratibu kimahaba.

Kama kuna baridi na wewe umevaa koti, jacket au sweta unaweza ukavua na kumpa; “Kuna baridi kali sana dear, vaa hili sweta,” kauli kama hii inaweza kuonyesha ni kiasi gani unavyomjali na kumpenda.

Wakati mwingine mnaweza mkawa mmekwenda ufukweni, katika maporomoko ya maji, msituni au hotelini, usijisikie vibaya kumbusu kila wakati, kuonyesha ni kiasi gani unavyompenda. Kwa ujumla mashamsham ni muhimu sana kwa ajili ya kumpagawisha boyfriend au girlfriend wako.

3. KIU YA MAPENZI
Hapa sitazungumizia kwa kirefu sana ila tutawekana sawa kidogo, unachotakiwa kumfanyia mpenzi wako ni kukata kiu yake ya mapenzi ipasavyo! Unaweza kufanya hivyo kwa kuwa mbunifu kila kukicha muwapo katika bustani nzuri ya wapendanao. Wanawake wengi huogopa kuonyesha uwezo au utundu wao wanapokuwa katika bustani hiyo maridhawa kwa kuhofia kuonekana hawajatulia!

Asikudanganye mtu, muwapo katika bahari ya wapendanao, kila mmoja ana wajibu wa kumridhisha mwenzake na kuhakikisha kuwa kiu yake inakatika kisawa-sawa. 

Kadhalika kila mmoja ana haki ya kufurahishwa na kukatwa kiu yake ipasavyo! Huo ndiyo ukweli wa mapenzi, inatupasa kila mmoja kufahamu ukweli huo na kuufanyia kazi.

Staili zakupagawishana kwenye majambozi kipindi cha ujauzito!




Bila shaka kila aliyeko kwenye mapenzi ana kiu yakufahamu staili mbalimbali atakazotumia katika uwanja wa huba kumpagawisha mwenza wake, kimsingi kuna staili nyingi sana ijapokuwa nyingi huhitaji wapendanao wawe wanasarakasi yaani wawe wepesi wa viungo.

Leo nitazungumzia staili ambazo mwanamke mjamzito anaweza kutumia na mwenza wake wakiwa katika huba na kumfanya afurahie tendo la ndoa na panapo majariwa nitazungumzia staili nyingine ambazo kila mmoja wetu anaweza kutumia katika majambozi kumpagawisha mwenza wake.

Kuinama: Hapa mwanamke anapaswa kuinama na kushikilia ama kiti, kitanda au kitu chochote kitakachomfanya asichoke miguu yake wakati mwanaume atakapokuwa akimwingilia kimwili. Hii ni staili nzuri kwa mwanamke mjamzito kwani mwanaume hataweza kulisukuma tumbo lake.

Hata hivyo, staili hii ina tatizo moja, uume wa mwanaume hauwezi kukisugua kinena na ikumbukwe kuwa mwanamke ili aweze kufika kileleni lazima mwanaume asiwe mvivu kukishughulisha kinena cha mwanamke kwani ni moja kati ya sehemu kuu ya mwanamke inayoamsha hamasa ya mapenzi na msisimko wa ajabu unaompelekea mwanamke yoyote yule kufika kileleni!

Hivyo, mwanaume hapa lazima ahakikishe anatumia mkono wake kumshikashika mpenzi wake kinena ili kumhamasisha kimahaba, lakini wakati anamshika mwanamke sehemu hiyo lazima ahakikishe vidole vyake si vikavu kwani endapo vitakakuwa havina unyevunyevu basi lazima mwanamke ataumia mara baada ya kupapaswa navyo katika kinena kwani kinena kimefunikwa na ngozi laini hivyo mwanaume anapaswa kuhakikishwa vidole vyake haviwi vikavu ili kumwezesha kuaamsha hamasa yake ya mapenzi.


Kukaa: Mwanaume anakaa kwenye kiti kisha mwanamke anakaa kwenye mapaja yake, hapa uume wa mwanamke hautaweza kuingia wote hali itakayomfanya mjamzito asiumie na mjamzito mwenye mimba ya miezi 8 hufurahia zaidi staili hii kwani ikumbukwe kuwa katika kipindi hiki mtoto huwa tayari ameshuka, mwanamke huonekana kuchoka na kuelemewa na tumbo.

Hivyo kwa kuwa mtoto huwa ameshuka mwanamke husikia maumivu sana pindi mwanaume anapotumia staili Fulani Fulani ambazo humpa nafasi ya kuingiza uume wake wote kwani motto huwa ameshuka hali inayopelekea kusukumwa na uume wa mwanaume pindi unapoingizwa na hivyo kumsababishia mwanamke maumivu.

MUHIMU:
Ni kweli katika kipindi cha ujauzito wanawake wengi hujisikia kuchokachoka sana hali inayowafanya wasipende kushiriki tendo la ndoa, lakini hali huwa tofauti kwa wanaume wengi pindi wapenzi wao wawapo wajawazito kwani ni kipindi ambacho mwanaume hufurahia sana kushiriki tendo la ndoa na mjamzito kutokana na ukweli kuwa katika kipindi hiki mwanamke huwa na joto lakutosha sehemu zake za siri, joto ambalo humfanya mwanaume apagawe. 

Hivyo mjamzito anapaswa kuhakikisha anafanya kila analoweza kumpa mwenza wake unyumba isipokuwa tu endapo atakuwa ameshauriwa na daktari kutoshiriki tendo la ndoa kwa sababu za kitaalam!

Followers