The Love Blog

Mambo gani ‘humpagawisha’ boyfriend au girlfriend wako?

Unaishi na mpenzi ambaye humpendi? Upo katika uhusiano na mpenzi ambaye moyo wako hauna chembe ya mapenzi? Unadhani kuna mtu anakusumbua, anahitaji kuwa na wewe, lakini moyo wako hausemi chochote juu yake? Jibu lake ni rahisi sana, achana naye!

Ni uamuzi mgumu kidogo kuamulika tena kutoka kwa mshauri kama mimi, lakini kitaalamu, hupaswi kuwa na mpenzi ambaye humpendi! Ukiendelea kuwa naye kwa sababu za kimasilahi, kuna siku moja utalia! Utalia kwa kumkosa mpenzi wako baada ya kujiua atakapogundua kuwa huna mapenzi naye, au wewe unaweza ukapigwa au kupata madhara yoyote baada ya kufumaniwa na mtu mwingine.

Kimsingi sio busara kuwa katika uhusiano na mtu ambaye unaamini moyo wako haupo upande wake! Ishi na mpenzi ambaye usipomuona kwa saa kadhaa moyo wako unatetemeka, hayo ndiyo mapenzi! Kamwe usilazimishe kuishi na mtu kwasababu ana pesa, maarufu au shinikizo la mtu, moyo ukuthibitishie kuwa unamhitaji kweli awe wako.

Huo ni utangulizi tu, sasa tugeukie katika mada ya msingi ya leo, tunaangalia mambo yanayoweza kumfurahisha ‘kumpagawisha’ mpenzi wako. Kama upo na mpenzi ambaye unampenda kwa mapenzi ya dhati, lazima kila siku utakuwa ukifikiria umfanyie nini ili afurahi!

Huo ndiyo ukweli wa mapenzi ya dhati, sasa leo nataka kuzungumza zaidi na wale walio katika uhusiano ambao hawajaingia katika ndoa (boyfriend/girlfriend). 

Yapo mambo mengi ambayo huweza kumpagawisha mpenzi wako asikuchoke na siku zote akatamani kuwa na wewe. Ila nimekuandalia mambo muhimu zaidi kumi. Hebu tuanze kuyaangalia mambo hayo yanayoweza kumfurahisha mpenzi wako.


1. KUMFANYA MWENYE FURAHA
Kati ya mambo ambayo huweza kumpagawisha mpenzi na kumfanya ajisikie vyema muda wote, ni wewe kumfanya afurahi! Jiulize, kama wewe ndiyo mpenzi wake wa dhati wa moyo wake, unadhani ni nani anayepaswa kumfurahisha kila wakati kama sio wewe? Jibu mwenyewe…

Jambo la msingi ni wewe kujisogeza karibu yake kila wakati, yaani uwe sehemu ya maisha yake. Hilo linawezekana, unaweza kumtumia sms au waraka pepe akiwa kazini ukimtakia mchana mwema, kazi njema au mlo mwema. Ni kitu kidogo sana lakini kinachoweza kufanya uhusiano wenu uwe wenye furaha wakati wote.

2. MASHAMSHAM...

Umenisoma rafiki? Ninaposema mashamsham, namaanisha aina fulani ya mapenzi yenye vituko na michezo ya kimahaba! Ukiwa naye matembezini, usione haya kumshika mkono na wakati mwingine kumtania. Unaweza kumshika mkono na kuupapasa-papasa taratibu kimahaba.

Kama kuna baridi na wewe umevaa koti, jacket au sweta unaweza ukavua na kumpa; “Kuna baridi kali sana dear, vaa hili sweta,” kauli kama hii inaweza kuonyesha ni kiasi gani unavyomjali na kumpenda.

Wakati mwingine mnaweza mkawa mmekwenda ufukweni, katika maporomoko ya maji, msituni au hotelini, usijisikie vibaya kumbusu kila wakati, kuonyesha ni kiasi gani unavyompenda. Kwa ujumla mashamsham ni muhimu sana kwa ajili ya kumpagawisha boyfriend au girlfriend wako.

3. KIU YA MAPENZI
Hapa sitazungumizia kwa kirefu sana ila tutawekana sawa kidogo, unachotakiwa kumfanyia mpenzi wako ni kukata kiu yake ya mapenzi ipasavyo! Unaweza kufanya hivyo kwa kuwa mbunifu kila kukicha muwapo katika bustani nzuri ya wapendanao. Wanawake wengi huogopa kuonyesha uwezo au utundu wao wanapokuwa katika bustani hiyo maridhawa kwa kuhofia kuonekana hawajatulia!

Asikudanganye mtu, muwapo katika bahari ya wapendanao, kila mmoja ana wajibu wa kumridhisha mwenzake na kuhakikisha kuwa kiu yake inakatika kisawa-sawa. 

Kadhalika kila mmoja ana haki ya kufurahishwa na kukatwa kiu yake ipasavyo! Huo ndiyo ukweli wa mapenzi, inatupasa kila mmoja kufahamu ukweli huo na kuufanyia kazi.

Followers